HATARI: Deni la Juventus laongezeka mara mbili - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HATARI: Deni la Juventus laongezeka mara mbili

Juventus jana wametoa takwimu zao za mapato na matumizi ya mwaka ulioshia mwezi June. Repoti hiyo inaonesha kuwa deni la klabu hiyo limeongezeka mara mbili tofauati na hapo awali.

Deni hilo limefikia kiasi gani?


Deni la Mabingwa hao wa Serie A limeongezeka mpaka kufikia Euro milioni 309.8 sawa na $362M kutoka Euro milioni 162.5 za deni la mwaka uliopita.


Licha ya kubeba Serie A mara ya 7 mfululizo na kutolewa hatua ya robo fainali ya Uefa Juventus hali yao bado haijagangamala.
Vipi kuhusu faida na hasara walizopata?


Kutokana na deni lao kuwa kubwa hata faida waliopata pia imepungua hasa ukilinganisha na mwaka mmoja kabla. Baada ya kupata faida ya Euro milioni 42.6 kwa msimu wa 2016-2017, Juventus wametangaza kupata hasara ya Euro milioni 20 kwa msimu wa 2017-2018.


Kiungo wa klabu ya Juventus Sam Khedira ameongeza mkataba utakaomweka klabu hapo hadi 2021.Mapato ya klabu nayo vipi?


Mapato ya klabu yalianguka kwa asilimia 10 kufikia mpaka Euro Milioni 504.7.


Mchanganuo kidogo 2017/18:... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More