HATMA YA DHAMANA MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA TARIME KUJULIKANA NOVEMBA 23,2018 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HATMA YA DHAMANA MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA TARIME KUJULIKANA NOVEMBA 23,2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Novemba 23.2018 itatoa uamuzi wa kumfutia dhamana ama la Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko baada ya wiki iliyopita kutoa amri ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya watuhumiwa hao kufika mahakamani wenyewe na kujieleza.

Akitoa maelezo yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, Mbowe amedai kuwa anaiheshimu mahakama sana na anatambua kama kiongozi na kama raia nafasi ya Mahakama katika kusimamia haki kwenye taifa.

Amesema, ni ukweli usiopingika kuwa yeye na washtakiwa wenzake ni viongozi na wana majukumu mengi ya kiungozi ya kutendaji ndani na nje ya nchi.

Mbowe ameeleza kuwa Oktoba 28, alisafiri kwenda Washington DC kwenye mkutano wa Oktoba 30, mwaka huu na kwamba kwa ratiba yake alistahili kuondoka huko Oktoba 30, usiku na kurejea Dar es Salaam Oktoba 31 kwa ajili ya kuendelea na Kesi Novemba Mosi, mwaka huu lakini bahati mb... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More