Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa, mahari ni milioni 8 – MC Pilipili - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa, mahari ni milioni 8 – MC Pilipili

Mchekeshaji MC Pilipili amefunguka kwa kudai kwamba hajakutana kimwili na mpenzi wake mtarajiwa, Philomena Thadey ‘Mina’ toka aingie kwenye mahusiano na mpenzi wake huyo.Pilipili ambaye weekend hii amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo, amedai mapaka sasa hajakutana na mpenzi wake huyo mpaka wafunge ndoa.

“Ni kweli nimeokoka, ndio maana kwenye sherehe ya kuvishana pete hakukuwa na vinywaji vikali, hatuishi pamoja na mpenzi wangu ila huwa anakuja nyumbani kwangu kupika’’ alisema MC Pilipili kupitia kipindi cha Leo Tena.

Aliongeza, “Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa”

Katika hatua nyingine MC huyo amedai ametoa tsh milioni 8 kwaajili ya mahari.

‘’Mshenga aliniambia mahari ni Milioni nane, na tulifanya mazungumzo kidogo, hivyo hadi sasa nimetoa mill. tano bado milioni mbili ’’ alisema Pilipili.


The post Hatutagusana na mpenzi wangu hadi tufunge ndoa, mahari ni milioni 8 – MC Pilipili appeared first on Bongo5.co... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More