HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI KWA MKANDARASI - WAZIRI KAMWELWE

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amemtaka mkandarasi  Makapo Contractors and General Supplies co. Ltd anayejenga barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Dott Service Limited anayejenga barabara ya Mtwara- Mlivata KM 50 kukamilisha barabara hizo kwa wakati.Amesema  kuanzia sasa Serikali haitakuwa na muda wa kumwongezea mkandarasi atakayebainika amechelewesha ujenzi kinyume cha mkataba.“Nimeridhika na ubora wa kazi yenu ni nzuri ila ongezeni kasi ili manufaa ya kuwepo kwa barabara ya lami kwa wananchi wa Mtwara yalete matokeo chanya haraka”, amesema Mhandisi Kamwelwe.Amesema  barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Mtwara- Mlivata KM 50 ni sehemu ya barabara kuu ya uchumi Mkoani Mtwara yenye urefu wa KM 210 inayoanzia Mtwara mjini kupitia Mlivata, Nanyamba,Tandahimba, Newala hadi Masasi.“barabara hii ikikamilika kwa wakati itaufungua uchumi wa wakazi wa Mtwara kwa kuongeza fursa za ajira, kilimo na biashara”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe .Naye mkuu w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More