Haya ndio maoni ya Watanzania kuhusu mabadiliko ya ada wanazotozwa wasanii na BASATA - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Haya ndio maoni ya Watanzania kuhusu mabadiliko ya ada wanazotozwa wasanii na BASATA

Ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu BASATA watangaze mabadiliko ya tozo za ada za usajili kwa wasanii wa filamu na wale wa Bongo Fleva kumeibuka na maoni tofauti tofauti wengi wao ambapo wadau na wasanii wameonekana kupokea mabadiliko hayo kwa mtazamo hasi.Gumzo kubwa kwa wasanii sio gharama za usajili kwani gharama hizo zimeonekana kushuka kutoka tsh 75,000/= hadi 20,000, bali gumzo ni kwenye gharama za makato kwenye tangazo atakalofanya msanii husika na gharama za matamasha.


SOMA ZAIDI-BASATA watangaza mabadiliko ya bei za usajili, MaDJ na Wasanii wapumua, Makampuni bei juu


Kwa mujibu wa mabadiliko mapya kutoka BASATA kampuni itakayomtumia msanii itatakiwa kulipa tsh milioni 5 kwa kila tangazo itakalofanya na msanii husika.


Kufuatia mabadiliko hayo Bongo5 imekusanya maoni ya Watanzania wa kawaida na wadau wa muziki kupitia kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wao wameonekana kushangazwa na tozo hizo hasa ya milioni 5 huku wengine wakiwashauri BASATA kukaa upya na Wasanii na wadau wengine wameenda mbali na kuingiza suala hilo na mambo ya kisiasa.


ndamao Ni lazima mlipe Kodi wasanii, Haiwezekani mnatakata wakati Watanzania tunazidi kupauka na kuwa hohehahe….lazima wote tuisome namba.


chuwagift Mtanyoooka tu na muda ukifka nendeni mkaimbe tena mbele kwa mbele!! Kanyaga twende mjomba


daxiyeerico@basata.tanzania kwani basata ndo wanafanya tangazo au anafanya msanii kwani basata ndiyo management ya msanii siku hizi??


nyau_19 Suala la kutaka kampuni zilipe basata 5mil kwa kila tangazo ambalo watamtumia msanii ni kutaka kuzidi kuminya mianya kwa wasanii wetu kupata fursa ya matanzano……mimi nilidhani sababu wasanii wanalipa kodi basi kufanya matangazo na ayo makampuni ndio kutumika kwa kodi zao uko maana show zenyewe asaivi ndio kama tunavyo ona media hii haipatani na uyu basi uyu hana show kwenye media ile, tunawaua wasanii wetu. #IloveTanzania


nellyblive BASATA HAMJANIJIBU….. HIVI MNATAKA KUUWA WASANII….MNATAKA WAFE NA NJAA Haya Iyo Ilkuwa Njia Nyingine Ya Wasanii Kujipatia Kipato….. Big Up @nchakalih Kasaidia Wasanii Wote…. Wa Hip Hop Na Bongo Fleva Kuwa Na Usawa Kwenye Matangazo….. Mnataka Hizi Kazi Tukazifanyie Njee….. MLIKAA NA WADAU GANI HAMJANIJIBU.


chattslatest Hivi hapo mnalinda na kutetea maslahi ya wasanii au mmelenga kujinufaisha wenyewe kupitia juhudi za wasanii!!? Hamuoni Kama hayo makampuni yataanza kukwepa kuwatumia wasanii kwenye matangazo yao na wasanii mnaosema mnawatetea wakakosa fursa?wasanii waitishe mkutano wa Dharura, wakubaliane kwa Pamoja kuikataa Basata.. waende na Mahakamani…


— SALIM (@salim_alkhasas) July 11, 2018
Mimi Nasema Basata Kazeni Tena Ikiwezekana Ongezeni Zaidi Ya Hapo – Wanyonyeni Mpaka Kwenye Bonmarrow Ili Wawe Na Akili Kesho.Katika Watu Wanaoongoza Kwa Usaliti Hasa Kwenye Mambo Yanayowahusu Watanzania Wenzao Na Kujifanya Kama Hawaoni Wala Hawasikii Ni Hawa Wasanii Wa Bongo.


— handsome La kijiji (@ManenoIzaak) July 11, 2018
Napata hisia kwamba suala la BASATA ni staged na huenda hivi karibuni The Czar of Kolomije akaibuka mwokozi. Vyovyote iwavyo, 'wasanii wengi wa bongo' remain the most THICK & DEPLORABLE artists of our time.


— M A G I R I (@Kiganyi_) July 11, 2018
Kwanini isiwe PAYE(pay as you earn) nani akalipie 5m ambayo anaweza akalipia matangazo ya bidhaa yake/service/product Any Media?BASATA tunajua mnatupenda/mnawapenda wasanii na kazi zao na faida zake But hii tozo inahitaji mjadala shirikishi na wadau wote wanauhusika sio mtu mmoja


— Antu mandoza🇹🇿 (@missmandoza) July 11, 2018
Hakuna Habari iliyoniburudisha kama ya basata na wasanii, nadhani basata wangeongeza masharti ingekuwa poa sana, Hawa Wajinga wanaongoza kwa kuwapoteza Sana watanzania mradi wao washibe @KennedyMmari @MarekaMalili @ManenoIzaak


— Najjash Shiraz Al is'haaq (@Iskhaz999) July 11, 2018
Hivi hawa wasanii si ndio hawa wakiwa kwenye red carpets wakiulizwaga kuwa nywele shilingi ngapi wanasema 800K, video 80M, laki 8, suruali 350K, viatu 200k, cheni 1M, Miwani 100K au sio hawa ambao wanalalamika hivi sasa kuhusu tozo za BASATA ambazo kwao ni kama hela ya jojo.


— Theodory Faustine (@TheoGiyan) July 12, 2018
Mie nashauri Serikali yetu tukufu kupitia BASATA iongeze makali. Tozo hizi ni ndogo sana. https://t.co/HaRv15Lc6v


— 肯尼迪 Ole Mmari™ (@KennedyMmari) July 11, 2018
Wahujumu uchumi wanaishambulia BASATA.


— Samurai⚔ (@YusuphMdogo) July 11, 2018
Ndugu wasanii, mnaendelea vipi na vita yenu na BASATA? VITA yenu mmemuachia bwana au mnaipigana wenyewe? Waendelee kuwanyoosha au walegezee? 2020 bado mtatupigia kelele za "mbele kwa mbele" na kupiga push-ups nyingi? Basi nasema hivi, BASATA wanyoosheni hawa watu!


— Martin M. M. (@IAMartin_) July 12, 2018
nataka kujua wanachokunywa BASATA.. unalinda hadhi ya Msanii kw kutoza Milioni 5 kwa kazi ya tangazo? mnakunywa nini?


— SALIM (@salim_alkhasas) July 11, 2018
Hii nchi tuijenge wote coz ni yetu sote. Mnapoona ndege imekuja wasanii wengi wamepongeza ila linapokuja swala la BASATA kulamba kodi wanaanza kulalamika oooh! "Yale maisha ya insta sio maisha yetu halisi hivyo hatuna hela hivyo BASATA wasiyafuate yale" Hivi ndege zinunuliwe vp?


— Hancy Machemba 🇹🇿 (@hancymachemba) July 12, 2018
yan studio nilipie, kuandikisha kazi zangu nilipie, video nilipie kila kitu nilipie , napata dili katika kampuni napo mnataka milioni 5 taslimu hivi hawa basata huwa wanajisikia wakiongea au huwa hawajisikii? jaman … Wasanii nawaonea huruma sana aisee yan mnaonewa sana sio haki


— Diva (@Divathebawse) July 8, 2018nicodemgram Mnatoza million 5 hivi mnajua matangazo yenyw wanapewa bei gani, hii cyo haki kabsa


chattslatest Hivi hapo mnalinda na kutetea maslahi ya wasanii au mmelenga kujinufaisha wenyewe kupitia juhudi za wasanii!!? Hamuoni Kama hayo makampuni yataanza kukwepa kuwatumia wasanii kwenye matangazo yao na wasanii mnaosema mnawatetea wakakosa fursa?


Hata hivyo, baadhi ya wasanii wa muziki na waigizaji akiwemo Steve Nyerere, Wakazi na Nikki wa Pili tayari wamepinga tozo hiyo kwa kile walichoeleza kuwa tozo hiyo itaanza kupoteza dili za wasanii kufanya kazi na makampuni.


The post Haya ndio maoni ya Watanzania kuhusu mabadiliko ya ada wanazotozwa wasanii na BASATA appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More