HESLB yajipanga kuchota mbinu kutoka kwa wadau Lilongwe - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HESLB yajipanga kuchota mbinu kutoka kwa wadau Lilongwe

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru
Na Omega Ngole, Lilongwe, TAASISI za kiserikali zinazotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Afrika zinakutana kwa siku nne kuanzia kesho (Jumatatu, Septemba 24, 2018) mjini Lilongwe, Malawi katika mkutano ambao Bodi ya Mikopo ya Tanzania (HESLB) ikisema imejipanga kuchota mbinu za kuongeza ufanisi.
Mkutano huo wa kimataifa utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika na umeandaliwa na Shirikisho la Taasisi hizo linalofahamika kwa kifupi kama AAHEFA. Washiriki zaidi ya 160 kutoka nchi 11 na wadau mbalimbali kama Benki ya Dunia, USAID wanatarajiwa kushiriki.
Washiriki hao ni maafisa wa Serikali, Watendaji Wakuu wa taaasisi hizo zinazotoa mikopo na wageni waalikwa kutoka Tanzania, Kenya, Rwanda, Ghana, Uganda and Zambia. Wengine wanatoka Botswana, Lesotho, Namibia, Afrika Kusini na wenyeji Malawi.
Mkutano huo utafunguliwa kesho (Jumatatu, Sept 24, 2018) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Malawi Bw. Brig... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More