Hii ndio sababu iliyoifanaya Marekani kuanza kuondoa wanajeshi wake Syria - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Hii ndio sababu iliyoifanaya Marekani kuanza kuondoa wanajeshi wake Syria

Baada ya siku kadhaa za mvutano juu ya tamko la rais wa Marekani Donald Trump kwamba ataondoa majeshi yake nchini Syria, afisa mmoja wa kijeshi amesema hatua hiyo imeanza kutekelezwa huku akikataa kuizungumzia zaidi. Kanali Sean Ryan, msemaji wa muungano wa kijeshi  unaoongozwa na Marekani unaopambana na wanamgambo wa dola la kiislamu amesema mipango ya kuondoka kwa maksudi nchini Syria imeanza.

“Kufuatia wasiwasi juu ya usalama wa operesheni hii hatutajadili lolote juu ya maeneo au mienendo ya wanajeshi hawa,” alisema Sean Ryan. Bado hapajakuwa na taarifa zaidi kuhusu kuondoka kwa wanajeshi hao, magari mangapi yalioondoka au hata iwapo kuna wanajeshi kadhaa ambao tayari wameshaondoka nchini humo.

Kwa mujibu wa dw, Shirika la Uingereza la uangalizi wa haki za binaadamu lililo na makao yake nchini Syria na linalofuatilia hali ya kivita nchini humo limesema Marekani ilianza kuwaondoa wanajeshi wake tangu jana usiku. Shirika hilo, limesema msafara wa magari takriban kumi ulione... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More