Hii ndio sababu ya Bondia Mtanzania Mwakinyo kutaka pambano na bondia maarufu kutoka Uingereza Amir Kha. - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Hii ndio sababu ya Bondia Mtanzania Mwakinyo kutaka pambano na bondia maarufu kutoka Uingereza Amir Kha.

Mwakinyo mwenye umri wa miaka 23 ambae usiku wa Jumamosi aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumtandika Mwingereza Sam Eggington mwenye miaka 25 katika raundi ya pili amesema yupo tayari kupambana na Khan.Pambano la Mwakinyo na Eggington la uzito wa kati lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano kubwa la Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas. Khan alishinda kwa tofauti ya alama dhidi ya Vargas.Mwakinyo aliingia katika uga wa Arena Birmingham, jijini Birmingham Uingereza kama mbadala wa bondia mengine aliyetakiwa kupambana na Eggington kushindwa kufikia vigezo.


Wachambuzi wengi wa masuala ya masumbwi waliliona pambano hilo kuwa rahisi kwa Eggignton ambaye alikuwa na rekodi bora zaidi. Wakati Mwakinyo akiwa na rekodi shinda mapambano 11 na kupigwa mawili, mpinzania wake alikuwa ameshinda mapambano 24 na kupigwa manne. Eggignton pia ni bingwa wa zamani wa Uingereza, Ulaya na nchi za Jumuiya ya Madola.


KHAN V VARGAS PROMOTION,
ARENA BIRMINGHAM,
BIRMINGHAM
PIC;LAWRENCE LUSTIG
Super-Welterweight... Continue reading ->
Source: Bongo5Read More