HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA MKOBA ILI KUJENGA UWEZO HOSPITALI ZA RUFAA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA MKOBA ILI KUJENGA UWEZO HOSPITALI ZA RUFAA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeanza programu ya kutoa huduma kwa njia ya mkoba ili kujenga uwezo wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini hasa katika maeneo yenye upungufu wa watalaam au maeneo yenye watalaam lakini wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi katika fani mbalimbali. 
Hayo yameswa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha wakati anazungumzia huduma hiyo.
Amesema kuwa utoaji wa huduma hiyo ni sehemu ya mpango mkakati wa Hospitali iliojiwekea kuhakikisha inatembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma kwa wananchi ambao wangepewa rufaa kwenda Muhimbili kupata matibabu wakati huohuo ikijenga uwezo wa watalaam."Hospitali ya Taifa Muhimbili ina majukumu makuu matatu ambayo ni kutoa huduma za ubingwa wa juu, kufundisha na kufanya utafiti hivyo huduma kwa njia ya mkoba ni kiungo kikubwa cha jukumu letu hapa nchini," amesema Aligaesha.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More