Huenda tukamuona Hazard akitua Manchester United,afaunguka kuwa anahitaji kufanya kazi tena na Mourinho - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Huenda tukamuona Hazard akitua Manchester United,afaunguka kuwa anahitaji kufanya kazi tena na Mourinho

Ikiwa ni likizo ya takribani wiki mbili kwa takribani ligi zote duniani kupisha michuano mbalimbali pia michezo ya kirafiki katika timu za taifa,kumeibuka sakata lingine linalomuhusu kocha wa Man United Mreno Jose Mourinho.Kocha huyu amekumbwa na misukosuko mingi sana tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza zingine zikimuhusu yeye na wachezaji wake lakini zingine zikimuhusu yeye na viongozi wa timu hiyo.


Moja ya mgogoro uliopo katika klabu hiyo ni ule unaemuhusu yeye na kiungo wa klabu hiyo Mfaransa Paul Pogba,ambao wamekuwa hawana maelewano kwa muda sasa,mgogoro huo ukichangiwa na kile kinachosemekana mchezaji huyo kunyang’anywa usaidizi wa unahodha katika klabu hiyo baada ya kuongea maneno yanayohusishwa na kuuponda mfumo wa uchezeshaji wa Mreno huyo.Sakata hilo likiendelea kunguruma katika klabu hiyo kubwa kabisa duniani,siku ya leo limeibuka lingine linalomhusu kocha huyo,ikiwa ni takribani miaka minne tangu kocha huyo kufukuzwa katika klabu ya Chelsea kwa ki... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More