HUMUD ASEMA ANA MKE MZURI KULIKO WACHEZAJI WOTE NCHI HII HAWEZI KUTONGOZA WAKE WA WACHEZAJI WENZAKE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HUMUD ASEMA ANA MKE MZURI KULIKO WACHEZAJI WOTE NCHI HII HAWEZI KUTONGOZA WAKE WA WACHEZAJI WENZAKE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIUNGO Abdulhalim Humud 'Gaucho' amesema kwamba ana mke mzuri kuliko wachezaji wa Tanzania hivyo, asingeweza kuwatongoza wake wa wachezaji wezake klabu ya KMC.
Humud amefukuzwa na klabu ya KMC kwa tuhuma za kuwatongoza wake na wapenzi wa wachezaji wenzake wa klabu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
Akijibu shutuma hizo, Humud amesema kwamba yeye mwenyewe ana familia ana mke na watoto hivyo hawezi kumvunjia heshima mke wake kwa kutongoza wake wa wachezaji wenzake. Abdulhalim Humud 'Gaucho' amekanusha tuhuma za kutongoza wake wa wachezaji wenzake

Alisema kuwa kwanza yeye anamke mzuri sana kuliko wachezaji wote wa Tanzania, maana mke wake akisimama na wake wa wachezaji wezake hawawezi kumfikia, hivyo hawezi kuwa na tamaa ya kutaka wanawake wengine.
"Siwezi kumdhalilisha mke wangu kwani ni mzuri zaidi kuliko wake zao, hivyo inabidi kuheshimiana na si kuharibiana maisha kwa vigezo vya kusema kwamba ninawatongozea wake zao," amesema Humud.
Mchezaji huyo wa zamani wa Si... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More