Huu ndiyo mji uliyo na masikini wengi nchini Marekani, asilimia 62.4 ya wakazi wake huishi chini ya dola moja kwa siku - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Huu ndiyo mji uliyo na masikini wengi nchini Marekani, asilimia 62.4 ya wakazi wake huishi chini ya dola moja kwa siku

Wakaazi wa mji wa Escobares uliopo katika mpaka wa Mexico na Marekani haukuwahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani.

62.4% ya watu wa Escobares, katika jimbo la Texas ni masikini

Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

“Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu,” anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani.

Débora Hernández,mkaazi wa Escobares.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bi. Debora hajui kusoma na kuandika, anasema alijifungua watoto saba lakini ni mmoja kati yao aliyebakie wengine wote wamefariki.

Alipoulizwa nini kilichosababisha vifo vyao alisema “Sijui, na wala sikuambiwa kilichowasibu”.

Alipokuwa mdogo alipelekwa katika shule ya wanafunzi wanaohitaji huduma maalum. Japo alikamilisha masomo ya msingi hakujifunza lolote.

Licha ya hayo yote Debora amekuwa akiishi na mume wake ambaye hana kazi kwa miaka mitatu sasa.

98% ya wakaazi wa ni watu wenye asili ya Uhispania.

Paa la nyumba yao linavuja kukinyesha na hali yao ya... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More