Huyu ndio mrithi sahihi wa Karius na Mignolet Liverpool ? - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Huyu ndio mrithi sahihi wa Karius na Mignolet Liverpool ?

Klabu ya Liverpool kutoka nchini Uingereza iko mbioni kukamilisha usajili wa mlinda mlango nambari moja wa klabu ya AS Roma pamoja na timu ya taifa ya Brazil Alisson Becker kwa uhamisho unaokadiriwa kufikia Euro milioni 66.


Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga rasmi na klabu ya AS Roma mwaka 2016 akitokea Brazil katika klabu ya Sport Club Internacional.

Liverpool wamekuwa wakiitafuta saini ya mlinda mlango huyu ambaye ni miongoni mwa walinda mlango bora kwa sasa duniani.


Pia wamekosa imani na walinda mlango wake kwa kuonekana kuwa ni sababu ya klabu hiyo kutokufanya vizuri katika baadhi ya michuano hasa michuano ya klabu bingwa barani ulaya UEFA katika mchezo wao wa fainali dhidi ya Real Madrid ambapo mlinda mlango wao Loris Karius aliweza kufungwa magoli ya kizembe na kupelekea Liverpool kupoteza mchezo huo,hivyo wakaamua watafute mbadala wake.Huku mlinda mlango mwingine raia wa Ubelgiji Simon Mignolet akikosa imani mbele ya kocha wa timu hiyo Mjerumani Jurgen Klopp ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More