HUZUNI KUBWA KWA TAIFA,MIILI YA WATU ... RC MONGELA AELEZA NAMNA WANANCHI WALIVYOFANIKIWA KUOKOA WATU 40 WAKIWA HAI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

HUZUNI KUBWA KWA TAIFA,MIILI YA WATU ... RC MONGELA AELEZA NAMNA WANANCHI WALIVYOFANIKIWA KUOKOA WATU 40 WAKIWA HAI

* Ni katika tukio la kuzama kivuko cha MV.Nyerere, Mbunge wa Ukerewe aomba kivuko cha uhakika

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema msiba huo ni mkubwa na wa kitaifa huku akieleza kuwa wananchi wamefanya kazi kubwa kwani wao ndio wamefanikisha kupata kwa watu 40 walio hai.

Mongella amesema hayo leo mchana huu wakati akitambulisha viongozi mbalimbali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameongoza maziko ya Watanzania waliopoteza maisha kutokana na tukio la kupinduka kwa kivuko cha Mv.Nyerere.

Mkuu huyo wa Mkoa amemwambia Waziri Mkuu kwamba Septemba 20 mwaka huu saa nane mchana walipata taarifa za kuwa kivuko hicho kinazama na wao wakafika eneo la tukio saa 11 jioni.

Amesema baada ya kufika walikuwa wananchi wa eneo hilo tayari wamefanikiwa kuokoa watu walio hai 40 na hakika wananchi hao wamefanya kazi kubwa."Watu 40 wameokolewa na wananchi wa maeneo haya.Sisi wengine wote tumeokoa mtu mmoja tu jana.Hivyo wananchi hawa wamethibitisha uwezo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More