ICC yamkuta Ntaganda na hatia - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ICC yamkuta Ntaganda na hatia

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague, imemtia hatiani kiongozi wa waasisi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bosco Ntaganda, kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.


Kwa zaidi ya miaka mitatu Ntaganda alikuwa akikabiliwa na tuhuma za uhalifu wa kivita anaodaiwa kufanya nchini Congo.

Jaji, Robert Fremr alisema mahakamani hapo leo Jumatatu Julai 8, kuwa Ntanganda maarufu Terminator, amekutwa na hatia katika makosa 18 ikiwamo mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono na kuwatumikisha watoto wadogo katika jeshi.


Ntaganda mwenye umri wa miaka 45 alishtakiwa kwa kusimamia mauaji ya raia na wanajeshi wake katika eneo linalokabiliwa na machafuko na lenye utajiri wa madini la Ituri Mashariki mwa Congo mwaka 2002 na 2003.


Sehemu ya ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo unadai kuwa kiongozi huyo alikuwa akiwakata koromeo na kisha kutoa viungo vya ndani, kuchinja watu na kuwa kufanya utumwa wa kingono.


Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa pia Ntagand... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More