ICC yamtia hatiani mbabe wa kivita, Ntaganda  - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ICC yamtia hatiani mbabe wa kivita, Ntaganda 

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague imemtia hatiani mbabe wa zamani wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.


Niederlande Internationaler Gerichtshof Prozess Bosco Ntaganda Den Haag (Getty Images/AFP/ANP/B. Czerwinski)


Kwa mujibu wa Shirika la habari la DW, Ntaganda, ambaye alishikilia hana hatia wakati wa kipindi cha miaka mitatu ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela baada ya kukutikana na hatia leo katika mahakama ya kimataifa ya ICC.


Hakuonyesha hisia zozote wakati jaji aliyesimamia kesi hiyo, Robet Fremr, alipopitisha hukumu hiyo.


Ntaganda alitiwa hatiani mara ya kwanza mnamo mwaka 2006 na kuwa ishara ya kufanya uhalifu bila hofu ya kuchukuliwa hatua kisheria katika bara la Afrika, akihudumu kama jenerali katika jeshi la Congo kabla kujisalimisha mwaka 2013 wakati nguvu zake ziliposambaratika.


Ntaganda mwenye umri wa miaka 45 alishtakiwa kwa kusimamia mauaji ya raia na wanajeshi wake katika eneo linalokabiliwa na machafuko na lenye utajiri wa madini l... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More