IDADI YA WATU WALIOUNGUA KWA MOTO MJINI MOROGORO YAFIKA 100 - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

IDADI YA WATU WALIOUNGUA KWA MOTO MJINI MOROGORO YAFIKA 100

Na Mwandishi Wetu.
Idadi ya watu waliofariki dunia kwa kuungua moto katika ajali ya kulipuka lori la mafuta Agosti 10 Msamvu mjini Morogoro imeongezeka na kufikia 100.
Majeruhi watatu kati ya 18 waliokuwa wamelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamepoteza maisha jana Agosti 20.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema leo kuwa, kwa sasa wamebaki majeruhi 15 kati ya 47 waliopelekwa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Amesema majeruhi wote wapo ICU chini ya jopo la madaktari wa Muhimbili na wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kutoka Lugalo.
Eligaesha ametaja waliopoteza maisha kuwa ni Mazoya Sahani, Khasim Marjani na Ramadhani Magwila.
"Madaktari wanajitaidi bila kuangalia uyu kaungua namna gani, kiu kubwa ni kuokoa wenzetu, madaktari wanafanya kwa sehemu yao, Mungu nae ana sehemu yake, kikubwa tuwaombee waliobaki," amesema.Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More