IDARA YA UHAMIAJI ARUSHA YAKANUSHA KUPOKEA MALIPO MKONONI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

IDARA YA UHAMIAJI ARUSHA YAKANUSHA KUPOKEA MALIPO MKONONI

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani Idara ya uhamiaji imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kijamii kuwa idara hiyo inapokea malipo mkononi kutoka kwa wateja wakati inafamika malipo yote ya serikali hulipwa kwa njia za huduma za kifedha.
Kamanda wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha Mratibu msaidizi Samwel Mahirani ameyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake na kuwataka watanzania kuwaamini viongozi wao na kutoa taarifa za malalamiko bila woga
Amekemea vikali wale wote wanatumia mtandao kuichafua Idara hiyo kuacha mara moja na pia kutoa taarifa kwa uongozi pindi wanapoona hawa kuridhishwa na huduma kwani kuna vitengo mbali mbali na box la maoni haoni sababu ya kulizungumza mtandaoni.
“Taasisi zote za umma hazipokei fedha mkononi bali fedha zote za umma zinapokelewa kwa njia ya miamala ya kifedha ikiwemo benki na mitandao ya simu za mkononi” alisema Kamanda
Alisema kuwa Hapendezwi na wanaotum... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More