INDIA: Mtoto mchanga azikwa akiwa hai, Fahamu zaidi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

INDIA: Mtoto mchanga azikwa akiwa hai, Fahamu zaidi

Mtoto mchanga wa kike amepatikana akiwa amezikwa hai katika kaburi la kina kifupi kaskazini mwa India, mkuu wa polisi afichua kisa hicho.Abhinandan Singh amewaambia wanahabari kuwa mtoto huyo alipatikana na mwanakijiji aliyekuwa ameenda kumzika mtoto wake aliyefariki baada ya kuzaliwa.


Mtoto huyo aliyekuwa amewekwa ndani ya chunguu na kuzikwa katika shimo la futi tatu, amekimbizwa hospitali ambako anapokea matibabu.


Polisi imeanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.


“Tunajaribu kutafuta wazazi wa mtoto huyo kwani tunashuku huenda hatua hiyo ilifikiwa kutokana na idhini yao,” Bw. Singh aliwaambia wanahabari katika jimbo la Uttar Pradesh.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi, mwanakijiji mmoja wlimpata mtoto huyo alipokuwa akifukua kaburi la kumzika mwanawe aliyefariki baada ya kuzaliwa.


“Walipokuwa wanaendelea na shughuli ya uchimbaji kaburi kijiko cha kutoa mchanga katika shimo liligonga chungu kilichokuwa kimezikwa fiti tatu. walilopokitoa walipata ndani kuna mtoto,” Bw Singh... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More