“Ingekuwa masumbwi Taifa Stars isingepangwa na Uganda”-Kiemba - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Ingekuwa masumbwi Taifa Stars isingepangwa na Uganda”-Kiemba

Mchezaji wa zamani wa Taifa Stars Amri Kiemba amesema ingekuwa ni mchezo wa masumbwi timu Taifa Stars isingepangwa na Uganda kwa sababu timu hizo mbili hazipo kwenye mizani sawa.


“Naipongeza timu kwa matokeo yaliyopatikana, inawezekana kuna wengine bado wanabeza kwa kutokujua uzito wa timu ya taifa ya Uganda”-Amri Kiemba, mchezaji wa zamani Taifa Stars.


“Kwa kipindi chote ambacho nimecheza na timu ya taifa ya Uganda hasa inapokuja mechi ya nyumbani kwao huwa ni mchezo mgumu sana husan kwenye uwanja wa Namboole. Kwa matokeo yale nawapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kuwapa Uganda heshima yao.”


“Kwa aina ya mchezo tuliocheza tuliwaheshimu na kucheza kwa ufundi wa mwalimu. Ni kitu kizuri japo watanzania bado hawajajua sisi tupo wapi ndio maana tunapata tabu. Kwa Uganda ilivyo sasa hatupo nao kundi moja kwenye viwango vya soka sisi tupo nyuma tunahitaji kufika ilipo Uganda.”


“Ingekuwa ni ngumi tusingepangwa kundi moja lakini kwa kuwa ni soka ndio maana tunapangwa pamo... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More