Iran yatoa vitisho vya kivita ‘Tupo tayari kupigana na Saudi Arabia na vibaraka wao Marekani’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Iran yatoa vitisho vya kivita ‘Tupo tayari kupigana na Saudi Arabia na vibaraka wao Marekani’

Kufuatia shutuma zinazotolewa na Marekani kuwa Iran ndio imetekeleza tukio la kushambulia vituo viwili vikubwa vya mafuta nchini Saudi Arabia vya Saudi Aramco na Khurais, Iran imesema ipo tayari kwa lolote lile hata ikibidi kwa vita endapo mataifa hayo mawili yataendelea kuwachokoza.Jana Septemba 14, 2019 Shambulio la ndege zisizokuwa na rubani zimerusha mabomu katika hifadhi vituo hivyo vikubwa vya mafuta ambavyo vinazomilikiwa na kampuni ya serikali ya taifa la Saudi Arabia.


Kanda za video zilizovuja mitandaoni zinaonesha moto mkubwa katika eneo la Abqaiq ikiwa ndio hifadhi kubwa ya mafuta ya Saudia huku shambulio la pili likichoma moto hifadhi ya mafuta ya Khurais.


Tayari, Msemaji wa kundi la waasi la Houthi la nchini Yemen, Limesema kuwa ndio limetekeleza shambulio hilo kwa kurusha ndege 10 zisizo na rubani.


Msemaji waasi hao, Yahya Sare akiongea na kituo cha runinga cha al-Masirah, Ambacho kinamilikiwa na waasi hao amesema kuwa mashambulizi zaidi yanafuata katika siku za usoni.


... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More