IVORY COAST NA MALI NAZO ZAANZA VYEMA MICHUANO YA AFCON - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

IVORY COAST NA MALI NAZO ZAANZA VYEMA MICHUANO YA AFCON

BAO pekee la Jonathan Kodjia limeipa mwanzo mzuri Ivory Coast katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa Kundi D Jumatatu Uwanja wa Al Salam mjini Cairo, Misri.
mshambuliaji huyo wa Aston Villa ya England alifunga bao hilo dakika ya 64 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji wa Toulouse ya Ufaransa, Max-Alain Gradel.
Ushindi huo unawafanga Tembo wa Ivory Coast waanzie kileleni mwa Kundi D wakilingana kwa pointi na Morocco ambayo jana iliipiga 1-0 Namibia ambayo kama Afrika Kusini wanaeleka kwenye michezo ya pili wakiwa na maumivu ya vipigo vinavyofanana.

Jonathan Kodjia akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Ivory Coast bao pekee la ushindi 

Aidha, katika mchezo wa Kundi E, Mali iliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritania Uwanja wa New Suez.
Mabao ya Mali yalifungwa na washambuliaji Abdoulay Diaby wa Sporting Lisbon dakika ya 37, Moussa Marega wa FC Porto zote za Ureno kwa penalti dakika ya 45, kiungo Adama Traore I... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More