IVORY COAST, TUNISIA ZAKAMILISHA ROBO FAINALI AFCON 2019 BAADA YA KUZITOA MALI NA GHANA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

IVORY COAST, TUNISIA ZAKAMILISHA ROBO FAINALI AFCON 2019 BAADA YA KUZITOA MALI NA GHANA

TIMU za Ivory Coast na Tunisia zimefanikiwa kutinga Robo Fanali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuzitoa Ghana na Mali katika mechi za jana nchini Misri.
Ivory Coast ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya Nane Bora ya AFCON baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mali, bao pekee la Wilfried Zaha dakika ya 76 Uwanja wa New Suez akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Jonathan Kodjia wa Aston Villa, zote za England. 
Tunisia ikafuatia kuing’oa Ghana kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Ismailia. 
Mshambuliaji wa Esperance, Taha Yassine Khenissi alianza kuifungia Tunisia dakika ya 73 akimalizia pasi ya kiungo Wajdi Kechrida, kabla ya Rami Bedoui anayecheza naye wa Etoile du Sahel zote za nyumbani, Tunisia kujifunga dakika ya 90 na ushei kuisawazishia Ghana.Bao pekee la Wilfried Zaha limeipeleka Ivory Coast Robo Fainali AFCON 2019

Katika mikwaju ya penalti waliofunga upande wa Tunisia ni Naim Sliti wa Dijon, Wahbi Khazri za Ufaransa, Dylan Bronn wa Gent y... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More