JAFO AAGIZA USAFI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JAFO AAGIZA USAFI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewaagiza Viongozi wa Jiji la Arusha kudumisha usafi ili kulinda miundombinu ya barabara ambazo zimejengwa jijini humo kwa gharama kubwa. Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayo tekelezwa chini ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Katika ziara hiyo,Waziri Jafo hakupendezwa hata kidogo na uchafu uliooneka kutapakaa ndani ya mifereji hiyo ambayo imejengwa hivi karibuni chini ya mradi wa uendelezaji Miji mkakati (TSCP).
 Kufuatia hali hiyo, Jafo ameugiza uongozi wa jiji hilo kuunda makundi ya wamama na wajane ambao wapo tayari kufanya usafi ili kila kikundi kikabidhiwe barabara yao kwa ajili ya kuitunza huku wakipata kipato ambacho kinaweza kikawasaidia kulea watoto na familia zao. 
 "Barabara za lami nzuri pamoja na mifereji iliyojengwa na zinazoendelea kujengwa zimeonekana kujaa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha miundombinu hiyo kuharibika haraka,"amesema Pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya barabara inayojengwa Jijini Arusha Jafo alitembelea kituo cha afya Kaloleni kilichopokea shilingi milioni 400 kutoka serikali huu lakini alikuta ujenzi haujaanza. Kutaokana na hali hiyo Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kuanza ujenzi huo kabla ya kumalizika kwa wiki ijayo na ametaka ujenzi huo uwe umekamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu mbalimbali.Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa jiji la Arusha alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni kukagua ujenzi wa miundombinu.


Source: Issa MichuziRead More