JAFO AAGIZA WEZI WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA NDAGO WAKAMATWE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JAFO AAGIZA WEZI WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA NDAGO WAKAMATWE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida kupitia vyombo vya dola kuwasaka wezi wote waliiba vifaa vya ujenzi wa kituo cha afya Ndago wilayani huo na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. 
Jafo ametoa agizo hilo leo baada ya kufanya ziara katika Kituo cha afya Ndago ambacho ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopokea Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali lakini ujenzi wake haujakamilika hadi sasa kutokana na baadhi ya vifaa kuibwa na wananchi wasio waaminifu.Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonyesha kukerwa na uzembe wa usimamizi uliojitokeza katika ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Hata hivyo, pamoja na kuagiza kusakwa kwa wezi wa vifaa, Waziri Jafo ameiagiza Ofisi ya mkoa wa Singida kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja ili kubaini kama kuna watumishi waliohusika katika sakata hilo nao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Waziri Jafo amemuagiza Mkurug... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More