JAFO AKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA KITUO CHA MABASI MJI WA NJOMBE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JAFO AKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA KITUO CHA MABASI MJI WA NJOMBE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mji wa Njombe licha ya serikali fedha zote za gharama ya ujenzi huo  zaidi ya  Sh. bilioni 10.  

Ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu Desemba 2013 lakini hadi sasa haijakamilika.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi hiyo pamoja na upande wa usimamizi wa ujenzi huo na kudai kuwa umechelewa kukamilika kutokana na uzembe wao. 

“Hapo awali kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na MASASI CONSTRUCTION kwa kujenga awamu ya kwanza na ya pili ambapo katika awamu hizo  zimekamilika lakini kwa kuchelewa sana na kulazimika kutafutwa mkandarasi mwingine ili akamilishe awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa mradi huo,”amesema.


 Amebainisha kuwa awamu ya tatu Halmashauri ya mji wa Njombe wamempata mkandarasi mpya ambaye ni kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL na amesaini mkataba mwezi Mei 2018 na anatarajiwa kukamilisha ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More