JAFO AMUAGIZA MKANDARASI KUBOMOA SAKAFU ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JAFO AMUAGIZA MKANDARASI KUBOMOA SAKAFU ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amemuagiza mkandarasi anayekarabati shule kongwe ya sekondari ya Malangali iliyopo wilayani Mufindi mkoani Iringa kubomoa Sakafu iliyowekwa kwenye madarasani kutokana na kuwa chini ya kiwango.
Hali hiyo imetokea leo wakati Waziri Jafo alipokuwa mkoani Iringa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Akiwa katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefika katika shule hiyo na kukagua moja ya darasa ambalo tayari lilikuwa limekamilika na kubaini kuwa sakafu yake imewekwa chini ya kiwango baada ya kugonga gonga kwa viatu na kutokea nyufa. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemuagiza Mkandarasi huyo kubomoa sakafu hiyo na kuanza kazi upya.
Jafo ameoneshwa kukerwa na hali hiyo na kuagiza msimamizi wa kazi hiyo ambaye ni Wakala wa Majengo nchini(TBA) kuhakikisha sakafu hiyo inavunjwa na kujengwa upya katika ubora unaotakiwa.Shule ya Malangali ni miongoni mwa shule kongwe 89 ambazo serikali imeamua kuzikarabati upya ili ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More