Jafo awajia juu Jiji la Arusha juu ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Kaloleni - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Jafo awajia juu Jiji la Arusha juu ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Kaloleni

Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewajia juu viongozi wa Jiji la Arusha kwa kutaka kubadilisha matumizi ya Tsh Milioni.400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Ukarabati wa Kituo cha Afya Kaloleni, baada ya uongozi wa Jiji hilo kutaka kuzipeleka katika kituo cha Afya Moshono.  “Fedha hizi zimeletwa kwa Makusudi Maalumu na mimi nakifahamu kituo hiki cha Kaloleni najua mahitaji yake sasa mnapotaka kuhamisha fedha hizi na kuzipeleka Moshono siwaelewi” Alisema Waziri Jafo.Aliongeza kuwa "Fedha hizo zitumike kuboresha Kituo cha Afya Kaloleni kama maagizo ya awali yalivyokuwa hayo mabadiliko mimi siyaafiki". Alisisitiza kunawakati ni lazima nyie wataalam wa Jiji mjiongeze haiwezekani serikali ilete fedha kwaajili yakuwahudumia wananchi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa Kaloleni nyie mnataka kupeleka hela Kituo cha Afya Moshono sitaki kusikia.  Jafo ambaye alifanya ziara katika kituo hicho kwaajili ya kujionea kama kweli fedha hizo alizoagiza zitolewe katika kituo hicho zimeshaanza kutumika na kubaini tangu Juni 26 mwaka huu fedha hizo zilipotolewa hadi sasa hakuna ukarabati wowote uliofanyika.  Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dkt, Simon Chacha alikiri ni kweli fedha hizo zililetwa na walitaka kuzipeleka kituo cha Afya Moshono lakini kwa maagizo ya Waziri Jaffo watajenga jengo la X-Ray, sehemu ya kusubiria wagonjwa (waiting bay), jengo la kufualia na kukarabati chumba cha meno, dawa, maabara na mfumo wa maji taka.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwasili katika kituo cha Afya Kaloleni wakati wa ziara yake Jijini Arusha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt.Simon Chacha. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Kwanza kushoto) akikagua chumba cha huduma ya meno wakati wa ziara yake katika kituo cha Afya Kaloleni Jijini Arusha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia) akipata maelekezo toka kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kwanza kulia) akikagua ramani ya jengo la upasuaji na wodi ya wazazi iliyofanyiwa marekebisho kulingana na eneo la kituo kuwa  dogo kujenga kwa ramani iliyotolewa awali.


Source: Issa MichuziRead More