JAFO AWATAKA WATENDAJI WA MANISPAA ZA DAR ES SALAAM KUONGEZA KASI YA UTENDAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JAFO AWATAKA WATENDAJI WA MANISPAA ZA DAR ES SALAAM KUONGEZA KASI YA UTENDAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda na Mkuu wa wilaya Kigamboni Sara Msafiri kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo Kigamboni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka watendaji wote wa Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kuongeza kasi ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao. 
Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali katika Manispaa hiyo. 
Katika ziara yake leo ametembelea Manispaa ya Kigamboni na kukagua ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyo pamoja na ujenzi wa Kituo cha afya Kimbiji. 
Katika miradi hiyo, Waziri Jafo hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wa Miradi hiyo ya maendeleo huku akiagiza ujenzi wa Ofisi za Manispaa ukamilike kabla mwezi Januari mwaka 2019 ili waondokane na tatizo la kupanga kwenye nyumba ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More