JE WAJUA SIRI MASHUKA YA KIGOMA.! - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JE WAJUA SIRI MASHUKA YA KIGOMA.!

Mashuka yenye urembo wa maua ya kushonwa na rangi za kuvutia yamening'inizwa pembezoni mwa barabara na nje ya nyumba kama uzio, ni ishara inayoweza kukujulisha kuwa umefika Kigoma.
Ni katika mji mkongwe wa Ujiji uliopo Kigoma Kaskazini, Magharibi mwa Tanzania eneo ambalo ni zaidi ya kilomita 1000 kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam.
Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza, maana uwepo wa mashuka hayo si kwa ajili ya kujipatia kipato tu bali ni mila na desturi kama lilivyo vazi la khanga.Na kuchagua mashuka mazuri, unahitaji usaidi wa kujua majina na ujumbe uliopo kwenye shuka unalolichagua.
Kila shuka lina jina lake, ambapo mengi yamebatizwa majina ya watu maarufu, wakiwemo viongozi wa kisiasa kama Mbunge wa mkoa huo Zitto Kabwe, Obama, Magufuli, Lowasa, Wema Sepetu na mengine mengi.
Huku majina mengine yakiwasilisha wanyama na vitu mbalimbali kama vile Pundamilia, Tausi, Nanasi, samaki wa kigoma, mwanamke mazingira, jumba la maneno, msala, pembe la ng'ombe, mwiba na ka... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More