JENGO LA KITUO CHA UMAHIRI LAKABIDHIWA KWA WIZARA YA MADINI. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JENGO LA KITUO CHA UMAHIRI LAKABIDHIWA KWA WIZARA YA MADINI.


Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV KAGERA.
Miongoni mwa majengo saba ya Vituo vya Umahiri (Centers of Excellence) yanayojengwa hapa Nchini, chini ya Wizara ya Madini likiwemo jengo lililojengwa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, limekabidhiwa rasmi na kupokelewa na Waziri mwenye Dhamana Mhe. Dotto Biteko mapema Oktoba 04, 2019.
Jengo hilo lenye Orofa tatu, lenye thamani ya Sh. Bilioni 1.081 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyetaka kuona mabadiliko katika Sekta ya madini kwa kuweka mazingira wezeshi.
Akizungumza kabla ya kukabidhiwa jengo hilo, Waziri wa Madini  Dotto Biteko amepongeza usimamizi wa Jengo hilo kwa ujumla, huku akikumbusha nia ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutaka kujengwa kwa Vituo hivyo Saba, lengo likiwa kuifanya Sekta ya madini iwe sekta ya wadau na wachimbaji wa uhakika, na kuondokana na ujanja ujanja uliokuwa ukifanywa awali, kufuatia nia hiyo pamoja na mambo mengine tayari leseni 12000 zimefutwa na zitagawiwa Kwa wachimb... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More