JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO - NDITIYE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO - NDITIYENaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema Ujenzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) umekamilika, na Jengo linatarajiwa kuanza uendashaji mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Pia amesema amefurahishwa kwa kukamilika kwa jengo hilo ambapo ni la kisasa na huduma zake zake ni nzuri.
Akizungumza mara baada ya Ziara ya kukagua Jengo hilo , amesema katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika JNIA inachukua nafasi ya tano na nafasi ya sita kwa idadi ya abiria.
‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa Ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa Kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi nzuri zaidi Barani Afrika kwani ni Jengo la kisasa na litatoa huduma nzuri,’’ alisema.
Nae Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNIA), Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi wa Kiwanja hicho, alisema mara baada ya kukamilika kwa jengo la tat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More