Jeshi la polisi Arusha lazindua Mfumo mpya wa kukusanya madeni - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Jeshi la polisi Arusha lazindua Mfumo mpya wa kukusanya madeni

Na Woinde Shizza Globu ya Jamii.
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetambulisha mfumo mpya wa ukusanyaji wa Madeni ya Makosa ya usalama barabarani unaotumia kamera maalumu zenye uwezo wa kupiga picha na kutambua gari linalodaiwa.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana amesema kuwa mfumo huo mpya utarahisisha kutambua Magari yote yanayodaiwa kupitia kamera maalumu zilizofungwa barabarani zitakazo kuwa zikipiga picha na kuonyesha kiasi ambacho gari linadaiwa.
Kamanda Shana amesema kuwa Jiji la Arusha limepata  kamera tatu za kisasa zinazotembea na zimefungwa katika maeneo mbalimbali katika Jiji la Arusha na kwamba machine hizo zinauwezo wa kutambua  namba za Magari ya aina mbali mbali.
Mtaalamu wa kitengo cha IT kutoka makao Makuu ya jeshi la polisi nchini,ACP Mayala Towo amesema mfumo huo umeanza kutumika  jijini dar es salaam tangu mwaka 2015, na sasa unasambaa nchi nzima na lengo ni kuhakikisha fedha ya serika... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More