JESHI LA POLISI LAKAMATA MADUMU 859 YA MAFUTA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JESHI LA POLISI LAKAMATA MADUMU 859 YA MAFUTAKamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa akiwaonesha waandishi wa habari mafuta yaliyokamatwa Bagamoyo.
Na Mwamvua Mwinyi, BagamoyoJESHI la Polisi mkoani Pwani, limekamata madumu 859 ya mafuta ya kula yanayodaiwa kutolipiwa ushuru, yenye thamani takriban milioni 50, huko Chemchem kata ya Magomeni Bagamoyo.
Akithibitisha kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani hapo,Wankyo Nyigesa amesema ,madumu hayo yalikuwa yakisafirishwa na Christopher Emmanuel (32).
Alieleza kuwa, Christopher aliyasafirisha madumu hayo kupitia gari yake namba T.621 BCG aina ya fuso baada ya kukwepa kulipa ushuru kwenye moja ya bandari bubu Bagamoyo.
"Tunachunguza risiti zake za malipo kwani pia zina TIN namba tofauti, tunamshikilia mtu huyu pamoja na aliyeshirikiana nae kutoa Hassan Saidi mpemba huyu mkazi wa Bagamoyo."
Wankyo amesema, huo ni usafirishaji haramu na kutia hasara Taifa kwa kukwepa kulipa ushuru ama kodi,hivyo amewaasa wananchi kuacha biashara za magendo.
Kamanda huyo amefafanua, wafanyabiashara wanap... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More