JESHI LA POLISI LAKIRI KUMBAMBIKIA KESI MFANYABIASHARA TABORA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JESHI LA POLISI LAKIRI KUMBAMBIKIA KESI MFANYABIASHARA TABORA


Mfanyabiashara huyo ni yule ambaye juzi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga, alimzungumzia kuwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi walimbambikia kesi ya mauaji huko Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, alisema awali walipokea barua ya malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara huyo.
Alisema baada ya kupoka, Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilimtuma ofisa wake mwenye cheo cha juu kwenda Tabora kufanya uchunguzi na kwamba hadi sasa anaendelea kuukamilisha ili hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika.
"Mpaka sasa yuko huko, kiufupi kwa taarifa ya awali aliyotuletea ofisa wetu ni kwamba kulikuwa na ukweli kwamba mwananchi yule alikuwa ameonewa," alisema Msangi.
“Tunaamini na kuelekezwa siku zote tunapofanya kazi za polisi tuzifanye kwa weledi na kuzingatia misingi ya sheria, kama mtu amekwenda kinyume hatuwezi kukaa kimya, hatua stahiki zitachukuliwa lisijirudie tena,” alisema.
Awali, akizungumza na Nipas... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More