JESUS AFUNGA MANNE MAN CITY YAICHAPA BURTON ALBION 9-0 CARABAO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JESUS AFUNGA MANNE MAN CITY YAICHAPA BURTON ALBION 9-0 CARABAO

Gabriel Jesus akishangilia baada ya kuifungia Manchester City mabao manne dakika za 30, 34, 57 na 65 katika ushindi wa 9-0 dhidi ya Burton Albion kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England jana Uwanja wa Etihad.
Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya tano, Oleksandr Zinchenko dakika ya 37, Phil Foden dakika ya 62, Kyle Walker dakika ya 70 na Riyad Mahrez dakika ya 83.
Timu hizo zitarudiana Januari 23 Uwanja wa Eton Park huku City ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kwenda fainali ya nne ya Carabao Cup ndani ya miaka sita ambako itakutana na mshindi wa jumla kati ya Tottenham na Chelsea Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More