JKT TANZANIA YAAMUA KUZIPELEKA MKWAKWANI MJINI TANGA MECHI ZAKE DHIDI YA SIMBA NA YANGA LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JKT TANZANIA YAAMUA KUZIPELEKA MKWAKWANI MJINI TANGA MECHI ZAKE DHIDI YA SIMBA NA YANGA LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya JKT Tanzania imehamishia mechi zake mbili za nyumbani za Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya vigogo SImba na Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. 
Uamuzi huo unatokana na Uwanja wake wa nyumbani inaotumia sasa wa Meja Jenerali Isamuhyo ulioko Mbweni Dar es Salaam, kutokuwa na uwezo wa kuhimili wingi wa mashabiki wa timu hizo mbili vigogo nchini Tanzania.
Na Bodi la Ligi (TPLB) imebariki uamuzi huo JKT Tanzania kutumia Uwanja wa Mkwakwani Jijini kama Uwanja wake wa nyumbani kwa mechi zinazoihusu Simba na Yanga. 
Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo Boniface Wambura anaeleza sababu za uamuzi huo na kusisitiza kuwa timu zote zimekwishapewa taarifa.


Baada ya kucheza mechi nane, JKT Tanzania inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 14, sawa na mabingwa watetezi Simba SC waliocheza mechi saba na Mbao FC waliocheza mechi tisa. 
JKT Tanzania inatarajiwa kuteremka tena dimbani Uwanja wa Mkwakwani kumenyana na wenyeji, Coastal Union k... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More