JKT YAIPIGA KMC UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JKT YAIPIGA KMC UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Ushindi huo umetokana na bao pekee na la kujifunga la Ramadhani Madenge dakika ya 40 na sasa JKT Tanzania inafikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda hadi nafasi ya 13 hadi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
KMC inayofundishwa na Mrundi, Etienne Ndayiragijje inabaki na pointi zake 25 ikifikisha mechi 20 za kucheza na kuendelea kukamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
 
Mechi nyingine ya Ligi Kuu, leo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, bao pekee la mshambuliaji wake nyota, Said Dilunga dakika ya 58.
Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting ifikishe pointi 23 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 16, wakati Ndanda FC inabaki nafasi ya 17 na pointi zake 19 za mechi 19 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More