Joh Makini afunguka ishu ya wasanii wa kiume kuvaa vikuku ‘sijui kesho yangu ila sioni tatizo’ (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Joh Makini afunguka ishu ya wasanii wa kiume kuvaa vikuku ‘sijui kesho yangu ila sioni tatizo’ (+video)

Rapper Joh Makini kutoka Weusi ameeleza mtazamo wake juu ya wasanii wa kiume wa muziki nchini kuvaa vikuku ambapo kwa mtazamo wake amesema yeye hilo anaona kama ni staili tu.Joh akiongea na Bongo5 amesema kuwa wasanii ni watu ambao wanaishi na fasheni na style mbalimbali hivyo msanii kuvaa kikuku ni maamuzi yake na yeye anachukulia kawaida kabisa suala hilo.


Akiongelea kwa upande wake kama anaweza kuvaa amesema kwa sasa hawezi kukubali wala kukataa kwani hiyo ni mitindo tu kama alivyoamua kuweka rasta wengine wanatoboa pua na wengine wanavaa vikuku.


Wiki iliyopita msanii  wa muziki Diamond Platnumz aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana mguuni akiwa amevalia cheni maarufu kwa jina la kikuku jambo ambalo lilisababisha ashambuliwe na mashabiki wake mitandaoni.


SOMA ZAIDI – Mashabiki wacharuka Instagram kisa picha inayomuonyesha Diamond kavaa ‘kikuku’


The post Joh Makini afunguka ishu ya wasanii wa kiume kuvaa vikuku ‘sijui kesho yangu ila sioni tatizo’ (... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More