Johari Apendezwi na Wasanii Wanaomwita Mlevi - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Johari Apendezwi na Wasanii Wanaomwita Mlevi

Mwanadada mkongwe wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameeleza kukerwa na baadhi ya wasanii wenzake kumpa jina la mlevi na kudai wapo wengine wengi ambao wanalewa mpaka wanalala baa.

Akichonga na Za Motomoto News, Johari alisema anachukizwa na baadhi ya wasanii kumuona yeye ndiyo mlevi peke yake wakati akiamua kunywa huwa anakunywa kistaarabu na wala huwa hana ugomvi na mtu yeyote lakini anashangaa kujadiliwa kila kona kwa kuitwa mlevi.


Nashangaa sana kwa kweli, kunywa kwangu pombe basi wasanii wenzangu wananiona mimi ndiye mlevi kuliko wengine wote duniani wakati kuna watu kibao wanakesha na kulala baa wala hao wasanii hawawajadili sasa najiuliza ingekuwa nakunywa kwa hela zao ingekuwaje? Naomba waniache,” alisema Johari bila kuwataja majina wasanii hao.


Ikumbukwe kuwa hapo karibuni mwanadada huyo alilipotiwa kuwekewa  madawa katika kinywaji chake alipokuwa akipata kiywaji katika bar moja jijini Dar na kumuibia pochi yake iliyokuwa na vitu mbalimbali.


The post ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More