Jokate Amtaka Miss Tanzania Ajiandae na Matusi Ya Mitandaoni - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Jokate Amtaka Miss Tanzania Ajiandae na Matusi Ya Mitandaoni

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe na Aliyewahi kuwa mlimbwende wa Miss Tanzania Jokate Mwegelo amefunguka na kumuandaa kisaikolojia Miss Tanzania mwaka 2018 Queen Elizabeth na mitandao ya kijamii.


Siku ya Jumapili Tanzania ilipata Miss mpya wa kuliwakilisha Taifa Mrembo Queen Elizabeth na mara moja mitandao ya kijamii ilianza kutoa maoni yao kuhusu Mrembo huyo.


Jokate ameibuka na kumuelezea balaa la mitandao ya kijamii na namna inavyoweza kumbomoa au kumjenga ambapo cha muhimu ni uajasiri kwani watu watakuwa na maoni mengi juu yake.


Kwenye mahojiano na Global Publishers , Jokate alisema baada ya kushinda, Queen Elizabeth amekuwa staa mpya kwa hiyo ategemee kusikia mengi kutoka mitandaoni.Kikubwa unatakiwa kuwa tayari kupokea kila kitakachokuja kwako. Kwa sababu wakati mwingine unaweza kutukanwa kiasi kwamba ukatamani uachane na mitandao hiyo. “Lakini unatakiwa kufahamu hiyo ni hali ambayo inawakuta wengi wetu. Kwa hiyo kuwa mvumilivu na kwa upande wako itumie mitandao kwa manufaa ya jina ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More