JONGO ALIYETANGAZA MECHI TAIFA STARS IKIFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 1980 AFARIKI DUNIA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JONGO ALIYETANGAZA MECHI TAIFA STARS IKIFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 1980 AFARIKI DUNIA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mtangazaji wa zamani wa michezo Ahmed Jongo aliyefariki leo hospitali ya Temeke mjini Dar es Salaam.
Jongo alistaafu utangazaji wa Redio Tanzania, kwa sasa TBC 2005 na kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, mwili wa Jongo unatarajiwa kupumzishwa kesho Saa 7:00 mchana katika makaburi ya Tandika mjini Dar es Salaam.

Ahmed Jongo katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa kwenye mahojiano na Azam TV 

Na kwa niaba ya TFF, Karia ametoa pole kwa wafiwa, familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo.
“Nimepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Ahmed Jongo,kwa niaba ya TFF natoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki,hakika tutamkumbuka kwa umahiri wake wa kutangaza mpira wa miguu”.
Rais wa TFF, Karia amesema Jongo enzi za uhai wake alipokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alikuwa chachu ya Watanzania wengi... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More