Joseph Kusaga Ajibu Tuhuma Za Kumiliki Wasafi Tv na Radio - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Joseph Kusaga Ajibu Tuhuma Za Kumiliki Wasafi Tv na Radio

Mfanyabiashara maarufu na Mkurugenzi wa Vlouds Media Group Joseph Kusaga amejibu tetesi zinasombaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.


Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv, Joseph Kusaga amefunguka kuwa yeye anamiliki karibia vituo vyote vya radio za vijana hapa Tanzania.Hapana mimi sitakwenda huko, mimi  namiliki radio zote za vijana, radio zote za vijana mimi namiliki, kwa njia moja au nyingine, ukimuita Seba atakwambia umenielewa. Lakini labda ni kwa sababu ya kuongeza wigo, labda wigo wetu sisi unaweza ukawa hautoshi, mimi nashiriki kwenye industry yote ya burudani”.Lakini pia Kusaga alipoulizwa kuhusu umiliki wa Wasafi Tv na Radio hakutaka kuweka wazi kuwa anamiliki zote lakini badala yake alisema anamiliki redio nyingi za vijana hapa nchini ikiwemo Jembe Fm ya Mwanza na Safari Fm ya Mtwara.


Wiki iliyopita kwenye Gazeti moja Kuna taarifa ilichapishwa kwamba Mke wa Kusaga anam... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More