JULIO ASEMA, UWEZO WA ALI KIBA SIO WA NCHI HII. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JULIO ASEMA, UWEZO WA ALI KIBA SIO WA NCHI HII.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa uwezo wa kimpira wa msanii Ali Saleh Kiba ni wa kucheza soka la kulipwa la kimataifa nje ya nchi.
Hayo aliyasema baada ya kumalizika kwa mchezo wa hisani wa kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundi mbinu mashuleni uliopewa jina la NIFUATE baina ya Marafiki wa Ali kiba na Marafiki wa Mbwana Samatta.
Julio amesema kuwa, uwezo wa Ali Kiba ni mkubwa sana na mara nyingi amekuwa anamuomba amsajili katika timu anazofundisha ila mwenyewe hakuwa tayari kucheza soka la ushindani.
"Mara nyingu nimekuwa namuomba nimsajili katika timu nazofundisha na nikiwa namwambia kabisa kuwa asije mikoani kucheza ila timu inapokua inakuja Kucheza Dar es salaam atakua anacheza," amesema Julio.
Amesema kuwa anachokifanya Ali Kiba uwanjani ni kikubwa zaidi kuliko wachezaji wanaopewa hela nyingi katika timu za Yanga na Simba."Ali kiba kama anaamua kucheza soka la ushindani ndani ya mwaka mmoja basi mwaka unaofuata lazima akacheze nje maana a... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More