Julius Mtatiro ang’atuka CUF  ‘hitaji la nafsi yangu ni kujiunga na CCM’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Julius Mtatiro ang’atuka CUF  ‘hitaji la nafsi yangu ni kujiunga na CCM’

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ametangaza kuachana na chama hicho hii leo Agosti 11 na kuonyesha nia ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).Mtatiro ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari hii leo huku akitaja maeneo matano ambayo yamemfanya kujiengua na CUF na kuamua kuunga mkono juudi za Rais John Magufuli.


”Nilichoomba kukutana na nyinyi ni kutangaza mustakabali wangu katika siasa za nchi yetu. Ninauchambuzi binafsi katika maeneo mbalimbali ambayo mimi ninashiriki kama mwanasiasa, kama kijana na kama kiongozi,” amesema Julius Mtatiro aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF.


Mtatiro ameongeza ”Katika tafakari yangu hiyo nilipitia maeneo kama matano ambayo nimeyafanyia kazi. Eneo la kwanza niliangalia ushiriki na mchango wangu kwenyesiasa za chama cha wananchi CUF, eneo la pili ilikuwa ni mgogoro unaoendelea kukikumba chama cha wananchi CUF, eneo la tatu ambalo nimelitafakari kwaupana sana ni ushiriki wangu kama kijana ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More