JUMA NYOSSO KUTUA YANGA - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JUMA NYOSSO KUTUA YANGA


KUNA uwezekano mkubwa beki wa zamani wa Simba na Mbeya City, Juma Nyosso akasaini Yanga akitokea Kagera Sugar.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kwamba beki huyo tayari amekamilisha hatua zote za awali kilichobaki ni mambo madogo ili usajili huo ukamilike na atacheza Jangwani msimu ujao.

Hata hivyo, inadaiwa kwa sasa Yanga inaendelea na usajili wake kwa siri na baada ya kufikia malengo yao ndio wataanza kuwafichua mmoja baada ya mwingine.

Habari za ndani zinadai kwamba Yanga kutoka na hali ya uchumi kutokaa sawa, wanahofia kuwa wapinzani wao wanaweza kutibua dili.

“Lakini usajili wa beki huyo si kwamba Yanga imeishiwa bali na kuangalia uwezo na kiwango ambacho amekuwa nacho nyota huyo kwa muda,” alidokeza kiongozi mmoja.

Nyosso ni kati ya mabeki wenye uzoefu wa kutosha kwenye Ligi Kuu Bara akiwa ameshazichezea timu za Simba, Coastal Union, Mbeya City na sasa Kagera Sugar.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alipoulizwa wamefikia wapi na mchezaji huyo alizuga na kudai kwamba yupo bi... Continue reading ->

Source: Sports KitaaRead More