JUMAA AKABIDHI GARI YA WAGONJWA KWALA ILI KUPUNGUZA ADHA YA USAFIRI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JUMAA AKABIDHI GARI YA WAGONJWA KWALA ILI KUPUNGUZA ADHA YA USAFIRI

Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha Vijijini
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi gari la wagonjwa (ambulance ),iliyogharimu mil.75 ,katika kituo cha afya cha Kwala .

Gari hiyo itaendelea kusaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa hasa mahututi na warufaa.Akikabidhi gari hilo ,kwa mganga mfawidhi wa kituo hicho ,diwani wa kata ya Kwala, mbele ya wananchi ,Jumaa alisema ataendelea kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao .

"Serikali yetu inafanya makubwa katika kupunguza changamoto mbalimbali kwenye sekta ya afya na nyingine kama elimu ,miundombinu na nishati ya umeme""Kwa kutambua hayo ,July 2017 nilikabidhi magari mawili ya wagonjwa yaliyotokana na mfuko wangu na jingine moja ni msaada kutoka kwa Rais John Magufuli ikiwa ni kati ya magari ya wagonjwa 67 yaliyogawanywa katika maeneo mbalimbali nchini" alisema Jumaa.

Hata hivyo Jumaa ,alisema ameamua kujikita kutatua kero mbalimbali ili kwenda pamoja na kauli mbiu yake ya SISI KWANZA SERIKALI BAADAE .Mbunge huyo ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More