JUMAA ATOA MISAADA KATIKA SEKTA YA ELIMU MAGINDU NA MUUNGANO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JUMAA ATOA MISAADA KATIKA SEKTA YA ELIMU MAGINDU NA MUUNGANO

 Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto )akimkabidhi mabati Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Magindu, Kasule Ambogo (mwenye kofia ) Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kushoto )akimkabidhi mabati Diwani wa kata ya Kilangalanga Mwajuma Denge.Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa (kulia)akimkabidhi jezi za michezo ,Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Mlandizi Kati ,Ally Nyambwilo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINIMBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Mkoani Pwani ,Hamoud Jumaa ametoa mabati 60 kwa ajili ya kuezeka darasa moja chakavu katika shule ya msingi Magindu .
Aidha amekabidhi sh. mil.mbili ambayo imenunuliwa bati 56 zitakazotumika kuezeka darasa jingine moja kati ya madarasa manne chakavu kimiundombinu yaliyopo shuleni hapo .
Pamoja na hayo ,Jumaa amechangia matofali 1,000 na mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kata ya Boko ,kijiji cha Mpiji .
Akikabidhi mabati hayo ,kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Magindu ,Kasule Ambogo ,mbunge huyo alisema ,anatekeleza ahadi alizozitoa na kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha na kutatua changamoto za sekta ya elimu .
Hata hivyo ,alikabidhi mabati mengine 25 yanayokwenda kutumika kuezeka ofisi ya walimu shule ya msingi Muungano kata ya Kilangalanga .
"Pia tumefanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kata ya Boko ,kijiji cha Mpiji ,ambapo tumepata sh.milioni 7 ,tofali 5,274 ,kokoto gari tatu, mchanga gari moja na mawe gari saba" alifafanua Jumaa.
Jumaa alisema kuwa ,ataendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo hasa kwa kutatua changamoto na kero za jumla ili kuinua maendeleo ya jimbo hilo .
Kwa mujibu wake ,kufuatia harakati hizo amewahi kutoa kontena la vitabu mbalimbali vya kujifunzia 40,000 ambavyo viligawanywa katika shule za msingi na sekondari za jimbo zima .
Akipokea mabati ,Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Magindu ,Ambogo alishukuru na kumuomba Jumaa kutochoka kusaidia changamoto zinazowakabili .
Ambogo alisema ,kwasasa wanategemea shida waliyokuwa wakiipata wanafunzi inaenda kuwa historia .
Nae diwani wa kata ya Kilangalanga ,Mwajuma Denge alisema haijawahi kutokea Mbunge wa kuwashika mkono kwa namna hiyo .
Alishukuru msaada wa mabati 25 yatakayotumika katika ofisi ya walimu shule ya msingi Muungano kata ya Kilangalanga na sh .mil moja kwa ajili ya kumalizia ofisi hiyo.


Source: Issa MichuziRead More