Jumia kunogesha sikukuu ya Eid kwa kutoa mbuzi bure kwa wateja - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Jumia kunogesha sikukuu ya Eid kwa kutoa mbuzi bure kwa wateja

Dar es Salaam - Agosti 10, 2018. Waumini wa dini ya Kiislamu nchini na duniani kote wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha siku ya Jumanne ya tarehe 21 mwezi wa Agosti. Hata hivyo, hii ni tarehe inayokadiriwa kwa sababu siku rasmi inaweza kubadilika kutegemeana na kuonekana kwa mwezi wa Dhul Hijjah.

Eid Al Adha ni sikukuu ambayo husherehekewa na miongoni mwa Waislamu duniani kote katika kukumbuka sadaka aliyoitoa Nabii Ibrahim (AS) kutokana na imani aliyokuwa nayo kwa mwenyezi Mungu (SWT). Nabii Ibrahim alionyesha utayari wake wa kumtoa sadaka mwanaye wa pekee, Ismail, lakini baadaye Mungu alimtoa mwanakondoo ili awe mbadala wa sadaka. Mwenyezi Mungu alipendezwa sana na usikivu wa Ibrahim kwake na kuwataka Waislamu kukifanya kitendo hiki na imani iliyoonyeshwa kuwa sehemu ya maisha yao.

Hivyo basi, kila mwaka ifikapo siku ya 10 ya mwezi wa Dhul Hijjah, Waislamu wote duniani husherehekea sikukuu ya Eid Al Adha. Katika siku hii, Waislamu huchinja mwanakond... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More