JUVENTUS WATENGA PAUNI MILIONI 175 KUMSAJILI MOHAMED SALAH - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

JUVENTUS WATENGA PAUNI MILIONI 175 KUMSAJILI MOHAMED SALAH

Na Ripota WetuKLABU ya Soka ya Juventus wanajipanga kutoa kitita cha pauni milioni 175 ili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah(26). Taarifa kuhusu Juventus kujiandaa kumsajili mchezaji huyo wa Liverpool ambaye kwa sasa yupo kwenye ubora zinatokana na tetesi ambazo zimebainika kuwepo kwa mpango huo.
Wakati kukiwa na tetesi hizo, pia tetesi nyingine katika anga la soka zinaeleza kuwa hatma ya Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo.Tetesi hizo ni kwa mujibu wa Telegraph. Hata hivyo wakati ikisubiriwa hatma ya kocha huyo, inaelezwa kuwa wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha 'kurekebishana' katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kutokana na kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)
Naye Kocha wa Derby Frank Lampard amepuuzia uvumi kuwa huenda akarithi mikoba ya Maurizio Sarri endapo Chelsea itaamua kumfukuza. (Evening Standard) Wakati huo huo kuna tetesi zi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More